Radio Kwizera
Jukwaa la Matumaini - Sowing Seeds of Hope
ADMINISTRATION
Director:
Damas Missanga, SJ
Assistant Director:
Deusdedit Byebalilo, SJ
Programmes Officer:
ALEX MCHOMVU
ACC & Marketing Officer
Mr. Donatus Baltazar
Baadhi ya wakimbizi wanaoishi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma,Magharibi mwa Tanzania wameanza kupokea fedha taslimu shilingi elfu kumi kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika hatua za awali za kubadilisha mfumo wa sasa wa kuwapatia chakula kila mwezi.
Watu zaidi ya 1792 kutoka vijiji vya Mparambo ya kwanza na ya pili, Rukana ya kwanza na I ya pili, Munyika ya kwanza na Gabiro wilayani Rugombo mkoani Cibitoke, kaskazini magharibi mwa Burundi wametoroka makaazi yao kufuatia ukame na uhaba wa chakula.
Wengi wao wamekimbilia katika vilaya jirani za Mugina na Mabayi mckoani Cibitoke, lakini pia kusini magharibi mwa Rwanda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Raia hao wameondoka na baadhi ya mizigo yao, huku nyumba zikiwa zimefungwa.
Mashamba ya mahindi, mihogo na maharage yameharibika kutokana na na jua kali. "Mvua za kwanza ambazo zingelianza kunyesha mwezi Septemba mwaka jana bado zinasubiriwa," mkaazi mmoja wa kijiji cha Mparambo ya kwanza.
Katika mkoa jirani wa Bubanza baadhi ya raia wameanza kuuza mabati ya nyumba zao ili waweze kupata chakula.
Baadhi ya viongozi tawala wamesema kuwa wana hofu ya kuzuka kwa wizi na vitendo vingine viovu kutokana na njaa ambayo imeanza kubisha hodi katika mikoa hiyo.
Hivi karibu baadhi ya raia wa mikoa ya Kayanza na Kirundo walikimbilia nchini Rwanda kutokana na njaa ambayo imesababishwa na mashamba kuharibika kutokana na ukame.
Kwa mujibu la gazeti la Iwacu, tayari viongozi tawala katika mkoa wa Cibitoke wameanzisha zoezi la kuwatambua raia wanaokabiliwa na uhaba wa chakula pamoja na waathirika wa majanga ya asili ili waweze kuwasaidia.
Kampuni ya mtandao wa Facebook bado inazidi kujiingiza fedha za kutosha – Imetoa ripoti yake ya faida walioipata katika robo ya kwanza ya mwaka 2016.
Katika ripoti hiyo Facebook imetangaza kuingiza faida ya dola bilioni 3.49 na kuzidi makadirio yao waliojiwekea huku hisa zake zikipanda thamani kwa asilimia 2 baada ya biashara ya saa moja.
Mapema mwezi April mwaka jana kampuni hiyo ilitoa ripoti ya kuongezeka kwa mapato yake kutoka dola milioni 512 kwa mwaka juzi hadi mapato ya dola bilioni 1.5 kuanzia mwezi Januari na Machi mwaka 2016.
Wakati huo huo mahakama moja ya kijimbo nchini Marekani imeitaka Facebook kuilipa dola milioni 500 kampuni ya ZeniMax Media (inachapisha video games) ili iweze kuzindua Virtual Reality Headset.
Marafiki wa kanisa la Anglikana wilayani Ngara mkoani Kagera, wametoa msaada wa baiskeli 13 zenye thamani ya Sh2.08 milioni kwa wanafunzi yatima wa shule ya sekondari ya kata ya Rusumo B, ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwahi masomo shuleni hapo.
Mratibu wa mfuko wa Tumaini Alex Samoya Nyamkara alisema marafiki hao wanaotoka nchini Canada na kisiwa cha Gumsey cha nchini Uingereza ambao wanafadhili miradi ya kijamii kupitia Mfuko wa Tumaini na kwamba pia wamekabidhi madaftari 1400 yenye thamani ya Sh1.6 milioni kwa wanafunzi 60 wa shule ya sekondari Rusumo B, Keza na Nyakisasa.
Nyamkara amesema kupitia wahisani hao shule 22 za kata wilayani Ngara zimenufaika kwa kuboreshewa mazingira ya kufundishia na kujifunzia hasa kwa kujengewa matundo ya vyoo , matanki ya maji na miundombinu mingineyo huku wanafunzi hao wakipatiwa taa za umeme wa jua (solar) ili kujisomea usiku.
Alisema wanafunzi waliopatiwa baiskeli hizo hutembea umbali wa kilomita 14 kwenda na kutoka shuleni na huchelewa kuanza masomo ambapo baadhi yao hasa wanafunzi wa kike huacha masomo kwa kukumbana na vikwazo vya maisha wanaopata ujauzito katika umri mdogo na kukatisha ndoto zao.
Pia lisema shule ya sekondari ya Kabanga wanafunzi wanajengewa matundu 10 ya vyoo yenye thamani ya Sh.42 milioni, Shule ya sekondari Murugwanza wanajengewa matanki ya maji, na wanafunzi wanaofaulu kitato cha nne na cha sita ambao ni yatima wataendelea kupewa mikopo kusomea fani mbalimbali.
Wakizungumza na wanafunzi waliopokea msaada baikeli na madaftari kwenye shule hizo marafiki wa kanisa hilo kutoka kisiwa cha Gamsey nchini Uingereza Sofi Danford pamoja na Linda Winey wa nchini Kanada waliwataka wanafunzi kujifunza kwa bidii na kutimiza ndoto zao kupitia taaluma ya elimu.
WFP na Msaada wa fedha kwa Wakimbizi Nyarugusu/Kigoma.
Familia 300 zatoroka Makaazi kutokana na njaa - Cibitoke/Burundi.
Facebook yapata Faida kwenye robo ya mwaka 2016.
Msaada wa Baiskeli kwa-Wanafunzi Yatima-Ngara/Kagera.
ORGANIZATION CHART